BurudaniPicha

Picha: Kleyah afunga ndoa na mchumba wake wa miaka 7

Baada ya kuwa katika mahusiano yaliyodumu kwa miaka 7 na kufanikiwa kuweka uhusiano wao nje ya macho ya umma, msanii maarufu wa Bongo Kleyah amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye pia ni meneja mshirika, Mhandisi Barnabas Ndyanabo mjini Kampala, Uganda Septemba 10, 2016.

f77bcf4a-d3bc-4890-aa16-445930c441dc

Harusi ilifanyika katika hoteli ya kifahari ya Serena. Sherehe hiyo ilibarikiwa na mualiko wa wageni 100 ambao ni watu wa karibu sana wa familia na marafiki.

b963aa54-34d2-45d3-b1b7-f8c8f34be263

Bongo songstress huyo alivalia lulu beaded fascinator na lace Berta vilivyonogesha gauni maalum lililotengenezwa na designer maarufu kutoka nchini Afrika Kusini na lilikuwa kama mermaid silhouette na alivalia viatu vya Bradgley Mischaka.

0dfcc064-ea08-431b-8798-ad5e0d09c935

Barnabas alivalia Tuxedo maridadi. Mavazi haya yaliwafanya maharusi hawa kupendeza kupita maelezo .

9edfc912-b1e6-48ed-8ad6-a26ef5b9c007

Kleyah alisema, “Sisi tulitaka hii siku muhimu zaidi katika maisha yetu tusherehekee na watu wa karibu sana na familia na ndio mana tulialika watu 100 pekee na hatukutaka kufanya sherehe kubwa sana kwa sababu hii ni siku ya kuwa karibu na familia.”

359f7753-e092-4830-b9e9-5ea3be36b704

Kleyah anasema daima ataendelea na maisha yake ya kimuziki hata baada ya kufunga pingu za maisha. Kleyah ni mtu ambaye kila siku hupendelea kuweka maisha yake binafsi na si mtu apendae kujulikana kwa maisha yake ya binafsi ukizingatia ndio kwanza ameanza muziki hivi karibuni. Amekuwa akipendelea kujulikana kwa mafanikio yake ya kimuziki na ndio maana amekaa mwezi mzima hadi kuja kutoa taarifa hii.

3b2f3eb9-8602-4ea6-b00d-89073a4b9c7c

Wanandoa hao wenye furaha wamebarikiwa kuwa na binti mrembo wa miaka 4 aitwaye Eleanor. Baada ya ndoa amerejea kufanya muziki na pia ameahidi kufanya hits nyingi zaidi kwa kushirikiana na wanamuziki maarufu wanaojulikana ndani na nje ya Tanzania.

771fe676-1b0e-4a28-bad2-888e8f8bf333

Amewataka wapenzi na mashabiki wake kujiandaa kupokea kazi zake mpya.

https://www.youtube.com/watch?v=-VlBY73LBMk

4849a470-e920-4c3e-8373-357dbe14038d

67248afe-bb3a-4f4a-93ff-5be2f890e234

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents