Burudani

Picha: Kayumba ashinda BSS 2015

Mwimbaji kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, Kayumba Juma amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2015 katika kilele cha shindano hilo kilichofanyika Ijumaa hii kwenye ukumbi wa King Solomon, Dar.

Mshindi wa Bongo Star Search 2015, Kayumba akiomba dua baada ya kutangazwa kuwa mshindi
Mshindi wa Bongo Star Search 2015, Kayumba Juma akiomba dua baada ya kutangazwa kuwa mshindi

Licha ya Kayumba kushindia kitita hicho cha pesa taslimu, pia amepewa mkataba pamoja na wenzake walioingia top ten wa kusimamiwa kazi zao na Tip Tip Connection kwa muda wa mwaka mmoja.

Ushindi wa pili umeenda kwa muimbaji wa Arusha, Nasib Fonabo na nafasi ya tatu kwenda kwa Frida.

Ushindani ulikuwa mkubwa baada ya Fonaba na Kayumba kuingia top two lakini wengi wanadai kuwa uchaguzi wa wimbo wa kumalizia wa Kayumba ulimfanya amalize kwa kishindo. Muimbaji huyo aliimba wimbo wa Isha Mashauzi, na kuufanya karibu ukumbi mzima unyanyuke. Fonabo aliimba wimbo wa msanii wa Uingereza, Ed Sheeran.

Kayumba akikabidhiwa zawadi kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo.
Kayumba Juma akikabidhiwa zawadi kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo

Kayumba ambaye anadai ametoka kwenye familia duni alionekana kuwa kipenzi cha wengi kwenye fainali hizo.

Kayumba akiwa amekumbatiwa na Penny
Kayumba akiwa amekumbatiwa na Penny

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents