Michezo

Picha: Juventus yatawala tuzo za Gran Gala del Calcio msimu uliopita

Usiku wa Jumatatu hii katika mji wa Milan zilifanyika sherehe za utoaji wa tuzo za Gran Gala del Calcio katika ligi kuu ya nchini Italia, timu ya Juventus ndio imeongoza kuzoa tuzo nyingi zaidi.


Picha ya Higuain wa kwanza kulia akiwa na Dybala wakwanza kushoto wakipokea tuzo zao

Timu hiyo imefanikiwa kushinda tuzo ya timu bora ya Italia baada ya kutwaa taji la ligi kuu ya nchi hiyo kwa mara tano mfululizo huku pia ikitoa wachezaji nane katika kikosi cha timu bora ya ligi ya Italia kwa mwaka 2015/16 huku kocha wao Massimiliano Allegri akifanikiwa kushinda tuzo ya kocha bora na Leonardo Bonucci akishinda tuzo ya beki bora.


Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri

Hii ndio timu bora ya Italia kwa msimu wa 2015/2016.

Gianluigi Buffon (Juventus), Andrea Barzagli (Juventus), Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Kalidou Koulibaly (Napoli), Miralem Pjanic (Juventus), Paul Pogba (Manchester United, formerly of Juventus), Radja Nainggolan (Roma), Marek Hamsik (Napoli), Paulo Dybala (Juventus) and Gonzalo Higuain (Juventus)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents