Burudani

Picha: Joslin kuachia video yake mpya baada ya wiki mbili

Msanii wa kundi la Wakali Kwanza, Joslin aliyewahi kuhit na ngoma kama ‘Niite Basi’ anajipanga kuachia video ya wimbo wake mpya ambao ameshoot hivi karibuni.

14309892_1789832297906938_2250043915090526208_n

Wimbo huo ameupa jina la ‘Only You’. Mara ya mwisho muimbaji huyo aliachia wimbo wake wa Tesa Naye mwezi Mei mwaka 2014 aliomshirikisha rapper Stopa Rhymes.

14449231_1579180832389368_6214746896250961920_n

Kupitia mtandao wake wa Instagram, muimbaji huyo ameandika, “Yeah…the return of#Joslin…(ndoto yao)..” “Yeah…#Joslin you&i@charm_and_loyal_proya “ONLY YOU”..,” ameandika kwenye picha nyingine aliyoiweka kwenye mtandao huo.

14294885_516718601855510_8543762894704082944_n

Akiongea na Bongo5, muimbaji huyo amesema kuwa kwenye wimbo huo hakuna msanii aliyemshirikisha na video hiyo anatarajia kuiachia baada ya wiki mbili kama mipango yake ikienda sawa. Wakati huo huo Joslin amedai kuwa mipango yake ya kuzirudia nyimbo zake za zamani bado ipo pale pale kama alivyowahi kuahidi siku za nyuma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents