Burudani

Picha: Jay Z, Beyonce, Kanye West, Madonna, Rihanna, Alicia Keys na wengi waizindua Tidal kwa kishindo!

Jay Z ameanza mbio zake za kuutafuta ubilionea kwa namna nyingine tofauti na kufanya muziki.

2725FA7800000578-3018528-Everyone_has_signed_up_From_Madonna_to_Deadmau5_Kanye_West_and_J-a-17_1427753345811
Madonna, Deadmau5, Kanye West na Jay Z

Rapper huyo akishirikisha na orodha ya wasanii wenye ushawishi duniani, jana alizindua mtandao wake wa TIDAL, jukwaa la kwanza la muziki la dunia linalomilikiwa na msanii linalotoa nafasi ya kusikiliza mamilioni ya nyimbo kwa malipo ya mwezi.

2725F55A00000578-3018528-image-m-105_1427752761432
Rihanna, Nicki Minaj na Madonna ni miongoni mwa wasanii wanaoumiliki mtandao huo

Uzinduzi huo ulifanyika jana kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini New York, Marekani.

2725E4C900000578-3018528-image-m-107_1427752868303

Wasanii waliohusika kwenye uzinduzi huo ni pamoja Alicia Keys, Arcade Fire, Beyoncé, Daft Punk, Jack White, Jason Aldean, Chris Martin, Calvin Harris, J. Cole, Jay Z, Kanye West, deadmau5, Madonna, Nicki Minaj, Rihanna, na Usher.

2725EA4900000578-3018528-image-m-93_1427751659772

Wasanii wote hao watafahamika kama waanzilishi wa kampuni na kila mmoja atakuwa na hisa kwenye huduma hiyo.

tidal-launch-15

“Tumekuja pamoja mbele yenu katika siku hii, March 30, 2015 tukiwa na sauti moja kwenye umoja kwa matumaini kwamba leo itakuwa wasaa mwingine ambao utabadilisha muelekeo wa historia ya muziki,” alisema Alicia Keys.

2725DA5500000578-3018528-image-a-94_1427751687792
Alicia Keys

“Lengo letu ni rahisi. Tunataka kutengeneza huduma nzuri zaidi na hali bora kwa wasanii na mashabiki. Na hiyo ni ahadi yetu kwa ulimwengu. Azma yetu inaenda mbele zaidi ya biashara. Inaenda mbele ya teknolojia. Lengo letu ni kuhifadhi umuhimu wa muziki kwenye maisha yetu.”

2725DF4300000578-3018528-image-a-96_1427751937115
Jay Z akisaini mkataba wa Tidal

Jay Z alinunua kampuni ya Sweden iitwayo Aspiro kwa dola milioni 56 na kuzindua tena ili kuwa mshindani wa Spotify, Pandora, YouTube na huduma zingine za kustream muziki.

2725DFFD00000578-3018528-image-a-95_1427751871233

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents