Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Habari

Picha: Hussein Pambakali na bosi wa Sea Cliff walivyowasili central Ijumaa hii

By  | 

Watu 65 waliotuhumiwa kuhusika kwenye sakata la biashara ya Madawa ya kulevya na kutakiwa kuripoti Ijumaa hii central polisi kwajili ya upepelelezi, baadhi yao wameitikia wito huo huku wengine wakishindwa kuitikiwa wito huo.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyaanika majina wa watu 65 ambao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituoni hapo ijumaa hii.

Kamera ya Bongo5 iliwashuhudia watuhumiwa watatu maarufu ambao ndio waliofika kituoni hapo akiwemo mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azzan, Hussein Pambakali na mmiliki wa hoteli ya Sea Cliff. Wakati huo huo mfanyabiashara maarufu Yusuph manji na askofu Josephat Gwajima waliowasili kituoni hapo siku ya Alhamisi lakini bado wanashikiliwa na jeshi hilo la polisi kwaajili ya mahojiano zaidi.

Naye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ndiye aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na wafuasi wake wengi waliokuwepo kituoni hapo hakuweza kuwasili kituoni hapo. Tazama picha hapa chini za Hussein Pambakali na mmiliki wa hoteli ya Sea Cliff wakiwasili kituo cha kati cha polisi.

Hussein Pambakali aliyevaa kanzu (damu ya mzee) akiwasili kituo cha polisi cha kati na mwanasheria wake

Mmiliki wa hotel ya Sea Cliff akiwasili polisi

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW