Burudani

Picha: Hennessy yasherehekea miaka 250 ya mafanikio Jburg

WATANZANIA watatu ni miongoni mwa waalikwa wa sherehe za kutimiza miaka 250 ya mafanikio ya kuanzishwa kwa kinywaji maarufu kutoka Ufaransa, Hennessy, sherehe ambayo iliyofanyika Johannesburg, Afrika Kusini hivi karibuni.

Nas and CEO wa Hennessy Bernard Peillon kwenye Gala dinner New York kabla ya kuja Johannesburg
Nas and CEO wa Hennessy Bernard Peillon kwenye Gala dinner New York kabla ya kuja Johannesburg

Miongoni mwa washiriki hao ambao pia walijumuika katika kuonja kinywaji hicho ni pamoja na; Deogratius Kithama wa East Africa Televisheni, Idris Sultan ambaye ni mshindi mkuu wa onesho la Big Brother Africa 2014 na Mpiga picha, pamoja na Tanya Mulamula wa kampuni ya Studiored Public Relations ambao walialikwa kuwa sehemu ya uzoefu huo.

Idris Sultan na Shaffie Weru - Mtangazaji Mkubwa kutoka KISS FM Nairobi
Idris Sultan na Shaffie Weru – Mtangazaji Mkubwa kutoka KISS FM Nairobi

Watatu hao walipanda pipa moja kwa moja hadi Johannesburg ambalo ni jiji lililoteuliwa kama moja ya majiji matano pekee duniani kuwa mwenyeji wa Hennessy 250 Tour, ambalo ni onesho la sanaa katika kusherehekea kumbukumbu ya miaka 250 ya kinywaji cha Premium Cognac mwaka huu.

Deogratius Kithama - Mtangazaji wa NIRVANA NA Mwandishi wa Habari kutoka Kenya Susan Wong wakiwa nje ya Exhibition Johannesburg
Deogratius Kithama – Mtangazaji wa NIRVANA NA Mwandishi wa Habari kutoka Kenya Susan Wong wakiwa nje ya Exhibition Johannesburg

Sherehe hiyo ilichota wageni maarufu ikiwa ni pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Hennessy, Bw. Bernard Peillon; Balozi wa Dunia wa Hennessy, Maurice Richard Hennessy; mwigizaji na mwimbaji Nandi Mngoma; mwigizaji Nomzamo Mbatha, Maps Maponyane; mshindi wa BBA 2014 Idris Sultani; mnyange na aliyekuwa Miss Afrika Kusini, Vanessa Carreira; mwinbaji na mtunzi wa wa ki-Nigeria, 2Face; DJ wa muziki wa Hip Hop na mfanyabiashara, T-Bo Touch; mtangazaji wa televisheni, Lorna Maseko-Lukhele, pamoja na mtunzajimwenza wa tukio hilo na mtaalam wa kumbukumbu za Hennessy, Raphaël Gérard.

Idris Sultan akiwa Nje ya CIRCA Gallergy Johannesbrg kwenye Hennessy Exhibition
Idris Sultan akiwa Nje ya CIRCA Gallergy Johannesbrg kwenye Hennessy Exhibition

Aidha, wageni walialikwa kupata uzoefu wa Hennessy 250 Tour, sambamba na chakula cha jioni na uwasilishaji wa kinywaji cha Hennessy 250 Collector Blend hasa iliyozalishwa na Hennessy Master Blender na Taster Yann Fillioux kwa ajili ya sherehe hiyo kubwa.

Idris Sultan na CEO wa Hennessy Bernard Peillon
Idris Sultan na CEO wa Hennessy Bernard Peillon

Ikijengwa kwa kampeni ya kisanii ya Hennessy Artristry iliyozinduliwa mwaka 2014, ziara ya Afrika ya Hennessy 250 Tour inalenga kuwatangaza duniani baadhi ya wasanii wenye vipaji wa Afrika, kuchanganya mchanganyiko wa sauti kamilifu, uvumbuzi kuona, na kupata uzoefu wa kipekee, kuzungumzia hasa sanaa mchanganyiko ya Hennessy.

Idris Sultan na 2Face kwenye Gala Dinner
Idris Sultan na 2Face kwenye Gala Dinner

Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Hennessy, Bernard Peillon, aliweza kufika kituo cha nne ziara ya Hennessy 250 Tour duniani kote na kufanya kweli katika jumba zuri la sanaa la Circa Gallery huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Hennessy, ambayo ni bidhaa maarufu ya Kifaransa na inayouzika sana duniani, inasherehekea kutimiza miaka 250 huku ikiwa imetengeneza chupa chache za Hennessy 250 Collector Blend – ambayo imetengenezwa kwa uangalifu mkubwa sambamba na kufanyiwa utafiti kwa miaka 4 kabla ya kuingia sokoni.

Limited Edition Bottle of Hennessy _250 Collectors Blend_ specially created for this 250 Year Anniversary

Kinywaji cha Hennessy kimerudi mwaka huu kwa ziara iliyopewa jina la Hennessy 250 Tour; onesho la kusafiri la kisanaa ambalo litawezesha kutembelea majiji matano makubwa duniani kwa ajili ya kusherehekea miaka 250 ya ukuu usio na makosa, sanaa mchanganyiko na urithi wake.

Ziara hiyo imefanyika kwenye maeneo manne maarufu duniani mwaka huu, ikiwemo miji ya; Guangzhou, Moscow, na New York, onesho hilo lilitua katika jumba la sanaa lijulikamalo kama Circa Gallery katika Jiji la Johannesburg Agosti 21, 2015 huku fainali ikifanyika Jijini Paris, Ufaransa.

Mmoja kati ya waalikwa wa ziara hiyo, Tanya, amewataka watanzania kujiandaa kwa ajili ya matukio ya Hennessy ambayo yatafanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents