Habari

Picha: Femina Hip wafanya mkutano wao wa mwaka na kutoa tuzo kwa wanachama wake

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Femina Hip Jumatano hii limefanya mkutano wake wa mwaka wa shule mbalimbali za sekondari nchini ambapo umehudhuriwa na wageni kibao akiwemo Naibu Kamishna wa elimu, Nicholaus Burreta, Balozi wa Denmark, Einar H Jensen, Mwakilishi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez, Mwakilishi kutoka ubalozi wa Sweden-Helena Reutersward wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dr. Minou Fuglesang.


Kuanzia kushoto: (Lyen Charles) kiongozi wa timu ya FeminaHip Nguvu ya Binti, (Alvaro Rodriguez) mwakilishi wa One UN Tanzania, (Dr. Minou Fuglesang) Mkurugenzi na mwanzilishi wa Femina Hip, (Nicholaus Burreta) Naibu Kamishna wa elimu Tz, (Einar Jensen) Balozi wa Denmark Tanzania na (Helena Reutersward) mwakilishi kutoka ubalozi wa Sweden.

Katika mkutano huo shirika hilo pia limetolewa tuzo mbalimbali kwa vijana waliopo katika klabu za Fema.

Akiongea katika mkutano huo mbele ya waandishi wa habari, Dr. Minou Fuglesang amesema, “Femina Hip inaamini kuwa ‘ujuzi laini’ kama vile timu ya kazi, muhimu kufikiri, ujuzi kujitolea na mawasiliano, ni muhimu kukuza uongozi, wanaharakati na kuandaa vijana kufanya kazi kwa bidii.”


Mkurugenzi mkuu wa Femina Hip Dr. Minou Fuglesang akiwa na mmoja ya washindi wa tuzo ya Fema

Hawa ni washindi waliofanikiwa kushinda tuzo za Fema.

1.Best Fema Club Netwok of the year (Mwanza Federetion of Fema club)
2.Runner up best Fema Club Network of the year (Dodoma students and teachers)
3.Best network mentor of the year (Mwl. Christopher Mavunde)
4.Best Fema club mentor of the year (Mwl. Bryson Paul kutoka Ngweli Fema club – Ngweli sec school, Sengerema)
5.Best Fema club of the year (Kisihigh Fema club – Kisimiri sec school, Arusha)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents