Picha

Picha: Exclusive listening party ya wimbo wa Vanessa Mdee ‘Closer’

By  | 

DSC_2357 (600x402)

Jana katika kiota cha Java Lounge kilichopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam kulifanyika ‘exlusive’ listening party ya wimbo mpya wa Vanessa Mdee uitwao Closer.

Party hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali waliokuja kumpa shavu mtangazaji huyo wa Choice Fm na MTV Base.
Miongoni mwa maceleb waliohudhuria ni pamoja na Ommy Dimpoz, Jokate Mwegelo, watangazaji wenzie wa Choice FM Thandi Kathembe, Abby Abby Plaatjes na Evance Bukuku, Julio, producer Lucci, watangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu, Steve B, Dina Marios, DeeAndy na Sade.

Wengine ni Fezza Kessy, Reuben Ndege, Avid, Wakazi na Gosby.

Katika party hiyo Vanessa alielekea upande wa Dj katika Lounge hiyo na kuzungumza mambo kadhaa kabla ya kuucheza wimbo huo. Mdundo wa Closer ulisikika vema kwenye speaker za Java Lounge kiasi cha kuwafanya waalikwa kushindwa kujizuia kushangilia na kuomba urudiwe tena.

“Attendance imekuwa poa yaani halafu mimi sijaalika mtu personally kwahiyo kutokana na promo tulioifanya Choice FM na Clouds FM watu wamekuja,” alisema Vanessa.

“ So it’s nice kuna watu positive watu wanaosupport movement so am really excited they are here, bado tuko mwanzo, it’s very interactive, najua ni kitu ambacho hakijafanyika Tanzania before so napenda kuwa intimate na fans wangu, those people who are listening to the music, wana support, wanadownload , kujua maoni yao juu ya nyimbo so that why nimefanya hiki kitu.”

Vanessa amesema sababu ya kuachia wimbo wake mwenyewe kipindi hiki haitokani na jinsi watu walivyomkubali kwenye collabo alizofanya bali huo ni mpango uliokuwepo kwa muda mrefu.

“Market ya Tanzania ni kama haitabiriki, so I was a bit sceptical but namshukuru Ommy Dimpoz kwa kunishirikisha kwenye nyimbo yake pamoja na AY. Wao wanasimama peke yao lakini ni kama favour wamenipa kamba nicollaborate nao and I am grateful for that forever kwasababu wameniintroduce kwa audience yao.”

“Video ya Closer itakuwepo before March,” alisisitiza Vanessa.

Asilimia kubwa ya watu waliohudhuria hafla hiyo wamesema Closer ni wimbo mzuri utakaomfikisha mbali mtangazaji huyo.

“Kwakweli I am in love with this track,” alisema Tinashe aka Avid ambaye ni msanii wa R&B. It’s a beautiful song, the quality of production ni nzuri, sikutegemea local production ikawa at this level. Cha pili ni kwamba I think she is grown as an artist.”

“Closer ni wimbo ambao unapeleka Bongo Flava kwenye level nyingine,” alisema Fezza Kessy ambaye ni rafiki wake wa karibu na Vee. “It’s English na Kiswahili mix a bit kwahiyo unakuta wote tunaelewa kama watanzania na international pia wataelewa. It’s nice R&B, the arrangement, the vocals kila kitu you can tell kwamba imefikiriwa na ikawa executed vizuri, it’s a beautiful song.”

Akiuzungumzia wimbo huo naye Ommy Dimpoz amesema, “Siku ya kwanza amenisikilizisha Closer kilikuwa ni kidemo Fulani hivi kifupi ni siku ambayo tunatoka kurekodi Nai Nai kwahiyo I know that song kwamba nikajua kabisa hii single itakuwa kali, kikubwa zaidi nimeona ukubwa wa Vanessa sasa, yeye kama yeye.”

“Vanessa ni msanii mkali sana. Katika wanadada ambao kiukweli wanaimba hapa Tanzania ile ni hazina.”

Tazama picha mbalimbali za za party hiyo hapo chini:

Julio na Leah

Julio na Leah

Reuben Ndege na Vanessa

Reuben Ndege na Vanessa

Abby (kushoto), Avid (Kulia) wakiwa na rafiki

Abby (kushoto), Avid (Kulia) wakiwa na rafiki

Vanessa akiwa na rafiki

Vanessa akiwa na rafiki

Reuben na Lucci wakitaniana

Reuben na Lucci wakitaniana

DSC_2553 (600x402)

Ommy Dimpoz, Jokate na Wakazi

Ommy Dimpoz, Jokate na Wakazi

Ommy Dimpoz na Jokate

Ommy Dimpoz na Jokate

DSC_2562 (600x402)

Producer Lucci na Reuben

Producer Lucci na Reuben

Throne Boy

Throne Boy

Leah

Leah

Wakazi na Lucci

Wakazi na Lucci

DSC_2529 (600x402)

Kuanzia kulia: Throne Boy, Charles, Lucci na Leah

Kuanzia kulia: Throne Boy, Charles, Lucci na Leah

DSC_2481 (600x402)

Rapper akipiga freestyle kwenye beat ya Closer

Rapper akipiga freestyle kwenye beat ya Closer

DSC_2489 (600x402)

Vanessa

Vanessa

DSC_2403 (600x402)

DSC_2400 (600x402)

DSC_2399 (600x402)

Lady Haha wa Clouds TV

Lady Haha wa Clouds TV

Watu waliohudhuria wakitoa maoni yao juu ya Closer

Watu waliohudhuria wakitoa maoni yao juu ya Closer

DSC_2376 (600x402)

Vanessa akichukua maoni ya wimbo wake kutoka kwa Avid

Vanessa akichukua maoni ya wimbo wake kutoka kwa Avid

Thandi na Abby wa Choice FM

Thandi na Abby wa Choice FM

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments