Burudani

Picha: Dodoma yajiandaa kuzungusha Kikwetu Kili Music Tour

Wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake leo wanatarajiwa kushuhudia tamasha la Kili Music Tour litakalofanyika uwanja wa Jamhuri.

7
Muonekano wa jukwaa litakalotumiwa na wasanii katika uwanja wa Jamhuri

1
Joh Makini, Gnako na Ben Pol wakiwasili mkoani Dodoma

Tamasha hilo ambalo mpaka sasa limezunguka mikoa 6 litawakutanisha wasanii zaidi ya 10 katika jukwaa moja waliofanya vizuri katika muziki kwa kwa kipindi cha 2013/2014.

2.1
Khadija Kopa akiwa amezungukwa na kundi la mashabiki baada ya kuwasili Dodoma

Wasanii hao waliowasili Dodoma siku ya jana wamesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Dodoma wanapata burudani ambayo miko mingine imeishuhudia.

2
Wasanii wakisubiri kuingia katika interview ABM FM

Akihojiwa na kituo cha Dodoma FM, Ben Pol ambaye alianzia muziki mkoani hapo amesema siku zote anajisikia fahari kutoa burudani mbele ya mashabiki wa nyumbani na kuelezea namna wasanii wengine walivyo na ari ya show hiyo.

3
Wasanii wakiwa katika interview studio za Dodoma FM

Wasanii wengine wanaotarajiwa kupanda jukwaani ni Khadija Kopa, Mwasiti, Shilole, Rich Mvoko, Christian Bella, MwanaFA, Izzo Bizness, Joh Makini, Nikki wa Pili na Gnako Warawara.

5
Izzo Bizness akijibu moja ya maswali aliyoulizwa kuhusu show

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents