Burudani

Picha: Diamond, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz waenda Marekani kwenye tuzo za Afrimma

Tuzo za African Muzik Magazine Awards, Afrimma zinatarajiwa kutolewa Jumamosi hii Oct. 10 jijini Dallas, Texas Marekani ambapo Tanzania inawakilishwa na wasanii saba.

Diamond Afrimma

Baadhi ya wasanii wa Tanzania wanaowania tuzo hizo akiwemo Diamond, Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz tayari wameondoka nchini kuelekea Marekani kuhudhuria sherehe ya utoaji wa tuzo hizo.

vanessa Afrimma
“Asante Sana Tanzania nyie wapenzi wa mziki mzuri ndiyo mmetupa fursa hii ya kwenda kuwawakilisha Dallas, Texas kwenye tuzo za @Afrimma Off to Dallas.Texas for the @Afrimma awards with my brothers@diamondplatnumz and @bdozen #Tanzania” – aliandika Vanessa kwenye picha aliyopiga na Diamond na mtangazaji wa Clouds Fm, B-Dozen wakati wa safari ya Marekani.

Kabla ya tuzo kutakuwa na Official Afrimma Welcome Party itakayofanyika Ijumaa Oct.9 kabla ya tukio lenyewe litakalofanyika kesho yake.

Ommy Dimpoz pia amepost kuwa atakuwa na show nyingine Houston, Texas Ijumaaa hii.
“This Friday At Safari Club Huoston Texas with my all team PKP see u there#AfrimmaWeekend Holla!!! “

Wasanii wengine wa Tanzania wanaowania tuzo hizo ni Alikiba, Lady Jaydee, Khadija Kopa, na Mrisho Mpoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents