Burudani

Picha: Davido na Wizkid wafuta dalili za beef mpya kati yao, ni baada ya Davido kuandika tweet zenye utata!

Star wa Nigeria Davido jana (July 24) kupitia twitter alirusha mashambulizi kwa mtu ambaye hakumtaja kwa jina lakini inaaminika ni msanii. Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya watu wahisi kuwa ni ujumbe kwa star mwenzake Wizkid ambaye ndiye mpinzani wake mkubwa kimuziki nchini Nigeria, ambao kwa Bongo tunaweza kuwafananisha na Diamond na Alikiba.

Davido na Wizkid

Lakini mtandao wa Lindaikeji umepost picha inayofuta uwezekano wa tweet ya Davido kuwa ilimhusu Wizkid. Kwa mujibu wa mtandao huo picha hiyo ya Davido akiwa na Wizkid wamepiga jana (July 24) katika uwanja wa ndege wa JFK, New York, Marekani ambako kila mmoja kaenda kufanya show tofauti.

Hiki ndicho alipost Davido kabla ya picha hiyo kupatikana
tweet11
tweet21

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents