Burudani

Picha: Baada ya Wema na Penny kumaliza tofauti zao sasa waanza kushirikiana kwenye kazi

Baada ya staa wa filamu Wema Sepetu na mtangazaji wa radio VJ Penny weekend iliyopita kumaliza tofauti zao zilizowatenganisha kwa muda mrefu, hatimaye sasa wameanza kuwa karibu.

Wema na penny

Kupatanishwa kwao kulikofanywa na rafiki yao Junaithar aliyewaalika kwenye dinner ya birthday yake usiku wa Jumamosi, haukuishia hapo bali sasa wamerudisha ukaribu kiasi cha kuanza kutembeleana.

wema na penny2

Kupitia Instagram Wema ameshare picha hii mpya akiwa na Penny nyumbani kwake na kuandika:

“And the Saga continues… I must say I am a Happy Soul…. So at peace…. Kajisemea shem lake na nanukuu ” kwenye vitu flani vya PROJECT…..” @vjpenny04 @jumalokole2″

Penny naye alii-repost.

wema na penny3

Lakini ukaribu wao wa sasa unaonekana pia unahusisha kazi, kupitia akaunti ya mtu ambaye Wema amemtag kwenye picha hiyo @jumalokole2, naye alipost picha hizo alizopiga nao, na kuandika caption zinazoashiria walikuwa wanarekodi kipindi.

jumalokole2: “Watu makini tukifanya yetu new Project @wemasepetu @vjpenny04…..” na nyingine aliandika “Kwenye vitu flani vya PROJECT…..! “

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents