Habari

Picha: Awamu ya pili ya Kongamano la ‘Her Initiative’ lafanyika UDSM

Jumamosi, Novemba 26 kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) limefanyika kongamano la pili la ‘Her Initiative’ linalosaidia kuwaelimisha watoto wa kike kujitambua na kuwa wajasiriamali.

img_0773

Kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya HER INITIATIVE lilihudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya Dar es Salaam na wasichana wajasiriamali pamoja na wageni kadhaa wakiwemo, Idris Sultan, Vanessa Mdee, Sebastian Ndege, Irene Kiwia huku mgeni mwalikkwa akiwa ni Mbunge wa Jimbo la Handeni vijijini na Mbunge wa Bunge la Afrika, Mboni Mhita.

Akiongea na watu waliohudhuria kwenye kongamano hilo, Mhe. Mboni aliwataka wanafunzi hao wasikate tamaa iwapo watashindwa kufanikiwa kwenye biashara zao kwani hiyo ni moja ya njia ya kupambana kufikia mafanikio hayo huku akiwaahidi kuwa matarajio yake ni kuwa Rais wa Kwanza mwanamke hapa nchini.

img_0672

Mgeni rasmi, Mhe. Mboni Mahita akiongea na wanafunzi wa jasiriamali wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam

“Nilienda sehemu kuchukua fomu ya kugombea nafasi fulani, nikakutana na dada mmoja akaniambia hiyo nafasi unayoitaka haijawahi kushikwa na mwanamke, nikamwambia hiyo ndio ninayoitaka. Mwisho nilifanikiwa kushinda nafasi hiyo, ameongeza.

Naye Sebastian Ndege ambaye ni mmiliki wa Jembe Group amewataka wanafunzi hao kuacha kuyafungia mawazo yao kwenye boksi kwa kufuata kitu vitu kwa ajili ya kuwafurahisha wengine, lakini pia amewataka wajiamini kwenye jambo lolote. Aidha amewataka wasikate tamaa kwa kushindwa kwenye jambo moja kwani hata yeye aliwahi kufungua kampuni 22 lakini zote zilikufa na kubakia sita pekee ambazo ndio mpaka leo anazisimamia.

Aidha Millard Ayo amwwataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa iliyopo kwenye mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo kunaweza kuwaingizia fedha nyingi zaidi kama wanavyofanya baadhi ya watu kwenye mitandao hiyo.
Idris Sultan ameongezea kwa kuwataka wanafunzi hao wasijaribu kufanya kitu ambacho wasichokijua. “Usisogeze mguu kama hauijui njia,” amesema.

img_0565

Lydia Charles (Mwenyekiti Mstaafu) akimtambulisha Irene Enock kuwa Mwenyekiti mpya wa Her Initiative

Wakati huo huo taasisi hiyo imemtangaza Irene Enock kuwa Mwenyekiti mpya huku aliyekuwa Lydia Charles aliyekuwa Mwenyekiti wa taasisi hiyo akipata kazi kwenye taasisi ha Femina.

Tazama picha zaidi hapa chini.

img_0808

Sebastian Ndege (Mmiliki wa Jembe Group) akiwa na wadau wa Her Initiative

img_0534

img_0679

img_0733

img_0752

Mtoto wa Sebastian Ndege akitoa neno kwa wanafunzi

img_0743

img_0785

img_0524

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents