Burudani

Picha: Arsenal yatambulisha ndege mpya ya kifahari

Arsenal imetambulisha ndege mpya ambayo itakuwa inaitumia kusafiria kwenda kwenye mechi zake za ugenini za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ndege hiyo ni ya kifahari na ina kila kitu kinachohitajika ndani. Klabu hiyo iliionyesha ndege hiyo kwenye Instagram wiki iliyopita, aina ya Emir­ates Airbus A380 nje ikiwa im­epambwa na picha za mastaa watano wa timu hiyo; Hector Bellerin, Olivier Giroud, Santi Cazorla, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Ndani ya ndege hiyo, kila mchezaji ana kitanda chake huku wakiwa wamewekewa anasa kibao, zikiwemo chaneli za televisheni 2,500 na kila mchezaji ana TV yake.

Ndani kuna baa ya kisasa yenye vinywaji vya kila aina, vyoo na mabafu lakini pia maz­ingira mazuri ya kukaa.

The Gunners wataipanda ndege hiyo kwa mara ya kwan­za watakaposafiri kuifuata Bayern Munich mwezi ujao. Angalia picha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents