Michezo

Peter Crouch aingia katika rekodi ya EPL

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Stoke City, Peter Crouch ameingia katika orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza ya muda wote.

Goli alilolifunga mshambuliaji huyo Jumatano hii katika mechi ya ligi kuu ya nchi hiyo dhidi ya Everton limemfanya kufikisha jumla ya magoli 100 aliyofunga katika ligi hiyo.

Kwa sasa Crouch anashika nafasi ya 26 katika orodha hiyo huku mshambuliaji wa zamani wa Newcastle United, Alan Shearer ndiye anayeongoza kwa kufunga magoli mengi katika ligi hiyo ambayo ni 260.

Baada ya kuingia katika orodha hiyo, Crouch aliandika katika mtandao wa Twitter, “100 club ????????.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents