Habari

Video: People Magazine lamtaja Lupita Nyong’o ‘Mwanamke Mrembo Zaidi’

Filamu ya kwanza ya Hollywood ilimpa Lupita Nyong’o tuzo ya kwanza ya Oscar. Na sasa jarida la People limemtaja Mkenya huyo kuwa ndiye ‘mtu mrembo zaidi duniani’ kwa mwaka 2014.

wmb-600

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa uhariri wa jarida hilo, Jess Cagle Nyong’o alikuwa chaguo sahihi kukava issue ya jarida hilo la kutimiza miaka 25. “She is fantastic. There really was no contest this year. The way she carries herself with such grace and humility, it put her over the top. I just love her,” alisema. Jarida hilo liliwahusisha wasomaji wake kutaja mtu anayestahili kuchukua heshima hiyo mwaka huu na Lupita kupendekezwa na wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=CVLpgOOBgG0

Na sasa mrembo huyo ameungana na wanawake wengine waliowahi kukava issue ya kutimiza mwaka wakiwemo Julia Roberts, Michelle Pfeiffer, Beyonce Knowles, Drew Barrymore na Jennifer Lopez. Kwa miaka 25, jarida la People limekuwa likitoa heshima hiyo na ni wanaume watatu tu waliowahi kupata ambao ni Mel Gibson, Tom Cruise na Leonardo DiCaprio (1996, 1997 na 1998). Mwaka jana alikuwa muigizaji Gwyneth Paltrow.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents