Michezo

Payet anataka kwenda Marseille tu

Mchezaji wa klabu ya West Ham United Dimitri Payet taarifa zinadai kwamba anataka kurejea Marseille kwa sababu za kifamilia, kwa mujibu wa habari.

Payet amekuwa gumzo katika kipindi hichi cha usajali baada ya nyota huyo wa Kimataifa wa Ufaransa kuwaambia West Ham kuwa hataki tena kuichezea klabu hiyo katika harakati zake za kutaka kuondoka.

West Ham wamekataa kusikiliza ofa yoyote kwa ajili ya mchezaji huyo, ikiwa imeripotiwa kuwa wameikataa ofa kutoka Mareseille mapema Jumatatu.

Kocha wa West Ham Slaven Bilic amesisitiza kuwa Payet hataondoka klabuni hapo mwezi huu, na West Ham hawana papara kumuuza nyota huyo ambaye saivi ana miaka 29.

Kituo cha Sky Sports News kimeripoti kuwa Payet anatamani kurejea kwenye klabu yake ya zamani kwa sababu za kifamilia baada ya kuondoka Marseille mwaka 2015.

Habari zinadai kuwa Payet amekataa ofa tele za klabu za Uingereza na China ili aweze kurejea zake Ufaransa.

Hadi sasa hivi ofa kubwa zaidi iliyo tolewa na Marseille ni paundi milioni 20, lakini Wagonga Nyundo wanahitaji kiasi kikubwa zaidi ili kushawishika kumwachilia kiungo huyo anayetaka kuondoka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents