Michezo

Paul Scholes aitaka United kuwasajili Raphael Varane, Luka Modric na Paul Pogba

Star wa zamanai wa Manchester United Paul Scholes amesema klabu yake hiyo ya zamani iwasajili Luka Modric, Raphael Varane na Paul Pogba katika dirisha lijalo la usajili kama kweli timu hiyo inataka kurejesha mafanikio yake barani Ulaya Scholes aliyesema hayo katika United We Stand fanzine.

futa

Huku pakiwa kuna mabadiliko kadhaa yanatarajiwa kufanyika Manchester United kwa kusajili nyota wapya pamoja na kuwafungisha virago wachezaji waliochemsha, hii ikiwa ni pamoja na benchi la ufundi linaloongozwa na Louis van Gaal.

3229493400000578-0-image-a-22_1458041224589

Inaaminika kocha huyo Mholanzi atatimuliwa mwishoni mwa mismu huku nafasi yake ikihusishwa kwa karibu na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho.

Scholes, aliichezea United kati ya mwaka 1992 na 2013, amesema wachezaji hao ni sahihi katika kutibu baadhi ya maeneo yaliyoiangusha timu msimu huu. Raphael Varane anacheza beki ya kati wakati Luka Modric na Paul Pogba ni wakali wa safu ya kiungo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents