Michezo

Patrice Evra ametaja sababu iliyomfanya asirudi Man United kwenye dirisha dogo

Beki wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa amesajiliwa na Olympique Marseille, Patrice Evra amefunguka sababu iliyomfanya ashindwe kujiunga na United kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Awali Evra alionekana kukaribia kutua United kwa asilimia kubwa akitokea Juventus lakini mwisho wa siku mashabiki walishangaa wakipokonywa tonge mdomoni. Mchezaji huyo amesema kuna mtu mmoja ndio amemfanya yeye asirudi tena kwenye klabu hiyo ya Uingereza.

“Nilikuwa nakaribu kurejea Manchester United. Nilizungumza na Mourinho lakini kuna mtu mmoja jina lake nisingependa kulitaja, hakika hakupendezwa na wazo langu la kurudi. Hata mashabiki walikuwa na shauku na ingekuwa furaha, lakini kwa sababu niligundua kuwa wao [klabu] hawawezi kufanya chochote nikamwambia wakala wangu anitafutie timu nyingine,” Evra ameiambia Sky Italia.

“Marseille immediately won me over with their project and immediately created a great feeling. We only spent one day to close the deal. They really treated me like a God, making it clear they had a great need for me,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents