Burudani

Pasha anaamini kuachana na menejimenti yake kumemfelisha

Muimbaji aliyewahi kuhit na ngoma mbalimbali ukiwemo ‘Ni Soo’, Pasha amedai kuwa kuachana na uongozi uliokuwa ukimsimamia kwenye muziki ni sababu ya yeye kupotea kwenye muziki.

pasha-4

Pasha ameiambia Bongo5 kuwa alijiona anaweza kufanya kila kitu lakini kumbe ni jambo lisilowezekana.

“Hapo katikati kama miaka minne iliyopita nilikuwa nimetetereka kwa sababu nilikuwa nimetofautiana kidogo na menejementi yangu. Baada ya kutoa ngoma yangu ya 2007 ‘Ni Soo’ pale nikawa nipo mwenyewe, nashindwa kufanya vitu vyangu, nashindwa kujigawa, kazi zikawa zinanielemea mambo yakawa yanashindwa kutoka on time. Kwahiyo nikasema 2015 nitajipanga vizuri pamoja na kufanya vitu tofauti. Kwahiyo natumai sasa naweza kufanya vitu vizuri sana,” amesema Pasha.

Muimbaji huyo pia amedai kuwa muziki wa sasa umebadilika.

“Kiukweli kutokana na hali itokanayo na muziki wa zamani na wa sasa hivi ni tofauti. Watu wa zamani walikuwa wanapenda kusikiliza tu nyimbo nzuri, lakini sasa hivi kuna vitu vingi sana kwenye utunzi, watu wanataka video kali. Kwahiyo unaweza kutoa wimbo mzuri na usifanye vizuri kikubwa ni kuwaomba mashabiki wetu wa ukweli kusupport kazi zetu. Pia hivi karibuni nimetoa wimbo mpya na video, unaitwa Mahaba Niue.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents