Habari

Pamoja na vikwazo, tunaendelea kujenga, usife moyo

“Ni kazi ngumu, kuna mahangaiko mengi, wakati mwingine mambo hayaeleweki, mambo yanabadiLika na gharama ni nyingi. Kufanya kazi kwa nguvu na kijituma ndio moyo wa mjasiriamali, huna Bosi wala mtu wa kukufuatilia lakini unahitaji kupambana kufa na kupona. Unahitaji kupambana, angalia uwezo wako na udhaifu wako katika kila unachokifanya, wateja ndio bidhaa yako ya msingi ambayo hutakiwi kuipoteza.” – Jason Goldberg, CEO, Fab

Ninaendesha kampuni yangu ndogo na kwa mwaka mzima mambo hayajaenda sawa, hali ni ngumu, lakini jambo la muhimu ninaona heshima sana kufanya biashara hii.

Jambo la muhimu ni kwamba je ninajua kampuni yangu inatakiwa kwenda wapi?

Itagharimu kuwa na watu sahihi kuendesha kitu sahihi ili kiweze kwenda mahali sahihi. kitu ambacho kinanigharimu ni kufikiri ninaweza kwenda peke yangu na kuendesha kampuni peke yangu. Huo ni mtego ambao wafanyabiashara wengi wanaochipukia tunatumbukia huko. Ili uweze kufika unakokwenda unahitaji watu wa kwenda nao , kuna wale utakaoanza nao, wengine wataishia njiani, huko njiani wengine wataungana na wewe.

Kuna wale watakukatisha tamaa, washirika wako kibiashara wataingia na kutoka, wengine wataona wazo lako la biashara si zuri na kukupa mawazo yao. Kitu cha msingi unajua unachofanya?

lakini Bwana Jason anatoa wazo lake kwamba:

“ Watu sikuzote husema kwamba uwe na watu sahihi. Hicho ni kitu rahisi kabisa, ni watu sahihi kwa wakati wa huu ndio wanaohitajika, na si vinginevyo “

Kila mtu hupata fursa ya kuwa mjenzi au kuanzisha jambo fulani. Haijalishi ni kwa muda mfupi au mrefu wewe ni mjenzi wa jambo hilo, hicho ndicho kinachotokea kwa waanzilishi wa biashara ni kujenga hiyo biashara. Kama hujengi biashara unafanya nini? kama hujaribu- hushindwi-hufanikiwi na kujifunza kadri safari inavyoendelea. Je utatokaje hapo ulipo kuelekea kule unataka kwenda?

Hivyo marafiki zangu, endelea kujenga hizo biashara. Kama wewe una watu wawili au kumi na hata mia moja, jiulize kila siku  “kwanini niko hapa?” kumbuka uko hapo kutazama jana na kuendelea kujenga kitu kizuri kwa ajili ya kesho.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents