Michezo

Pambano la Tyson na Klitschko laahirishwa tena

Mpiganaji masumbwi ambaye ni bingwa wa uzani mzito kutoka Uingereza Tyson Fury ameahirisha tena pambano lake la marudiano dhidi ya Wladimir Klitschko kwa mara ya pili kwasababu ”afya yake hairidhishi”.

100748e700000514-0-image-a-41_1474655983601

Mapromota wake hawakueleza undani wa taarifa zaidi lakini wamesema ” hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo”.

Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana.

Marudio ya pambano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunja fupa la kisigino chake.

3396c49400000578-3804602-fury_was_out_of_shape_when_he_appeared_at_a_controversial_press_-m-43_1474656265962

Pambano jipya la marudio kati ya mabondia hao wawili lilipangwa kufanyika Octoba 29.

“Tyson sasa inabidi afanyiwe matibabu anayohitaji ili aweze kupona kikamilifu,” Hennessey Sports iliongeza.

“Tunaomba radhi kwa wote wanaohusika katika pambano hili na mashabiki wote wa masumbwi waliotazamia maruduo hayo. Ni wazi kuwa Tyson pia amehuzunishwa na hali ilivyo.

“Tutatoa taarifa zaidi katika muda unaofaa.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents