Burudani

‘Pale Kati’ imefanya vizuri kabla ya kufungiwa na BASATA – Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amefunguka kwa kusema kuwa kabla ya wimbo wake ‘Pale Kati’ kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) tayari wimbo huo ulishafanya vizuri katika sehemu mbalimbali za nchi.
nay new2

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii kabla ya kikao chake na BASATA siku ya Jumanne, Nay wa Mitego amesema hana tatazo na wimbo wake kufungiwa kwani tayari ulifanya vizuri katika sehemu mbalimbali.

“Unajua wimbo wangu tayari ulishafanya vizuri, na bado kuna redio zinaendelea kuupiga, sema mimi nachotoka ni uhuru wa wimbo wangu, kila mtu aupige akijisikia sio kwa ajili ya kumuogopa kitu fulani, lakini ‘Pale Kati’ umefanya vizuri kabla hata ya kufungiwa na BASATA” alisema Nay wa Mitego.

Rapper huyo pia amewataka mashabiki wake kuendelea kuusupport wimbo huo huku akiwataka kukaa mkao wa kula kwa ajili ya video za wimbo huo.

Wimbo huyo ulifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutokana na wimbo huo kudaiwa kukiuka maadili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents