Burudani

Pah One waeleza kwanini Navy Kenzo wamefanikiwa zaidi yao

Baada ya Nahreel na Aika kujiondoa kwenye kundi la Pah One na kuunda kundi lao la Navy Kenzo linalofanya vizuri kwa sasa, Pah One wamesema Navy Kenzo wamefanikiwa zaidi kutokana na kufanya kazi muda mrefu, tofauti na wao ambao walikuwa hawafanyi kazi kutokana na kusafiri sana.

PahOne

Wakizungumza katika kipindi cha ‘Siz Kitaa’ cha Clouds TV, Pah One wamesema kuwa sasa wamerejea na watafanya kazi ili wafike wanapohitaji.

“Kwa sisi ni kwamba sisi tulikuwa hatupo, wao walikuwepo wanaendelea na muziki,” walisema Pah One. “Kwahiyo mimi kitu ambacho nakiona wao wanafanya vizuri na sisi tutafanya vizuri kwa muda ambao tupo kwa sababu tumeanza kutoa kazi zetu. Tutafanya kazi tufike tunapotaka kufika na wao watafanyakazi wafike wanapotaka kufika,” Walisema Pah One.

Katika hatua nyingine Pah One amewataka Navy Kenzo kuacha kutengeneza chuki baina yao kwa kuwa kila kundi linafanya mambo yake na lina mwelekeo wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents