Michezo

Pacquiao na Mayweather wakutana hotelini kuzungumza, ni baada ya kuonana kwenye game ya Miami Heat

Mechi kati ya Manny Pacquiao na Floyd Mayweather huenda ikawepo.

_80569190_pacquiaomayweather_threetweet_grantsmitytwitter

Mashabiki wa ndondi Jumanne hii walijawa na furaha kubwa baada ya kuwaona mabingwa hao wakisalimiana baada ya kukutana kwa mara ya kwanza kwenye game ya Miami Heat.

Kwa mujibu wa mshauri wa Pacquiao, Michael Koncz, Mayweather alienda kwenye chumba cha hoteli cha Pacquiao kuzungumza uwezekano wa pambano lao la May 2.

“Kilikuwa ni kitu kizuri na cha kutia moyo sana, na tunamsifu Floyd kwa kuja,” Koncz aliiambia ESPN.com Jumatano hii.

“Hiyo ni mara ya kwanza wameonana. Nimewahi kukutana na Floyd mara nyingi lakini Manny hakuwahi kupata nafasi ya kukutana naye. Waliongea kwenye halftime, lakini huu ulikuwa mkutano serious na mrefu.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents