Diamond Platnumz

P-Square ni mashabiki wa ‘Nitampata Wapi’ na Mdogo Mdogo za Diamond

Unataka kuyakuna masikio ya P-Square? Usiimbe kwa kuchanganya na ladha ya Nigeria, imba Bongo Flava halisi! Hilo ndio somo ambalo Diamond amelipata wiki hii kutoka kwa Peter na Paul Okoye.

10895324_779474402147260_1370451255_n
Msanii wa kundi la P-Square, Peter Okoye akibadilisha mawazo na Diamond Platnumz

Diamond pamoja na wasanii hao nguli wa Afrika na wengine wakiwemo Flavour na Fally Ipupa watatumbuiza leo kwenye tuzo za wanasoka bora wa Afrika wa CAF 2014.

Inadaiwa kuwa baada ya hitmaker huyo wa ‘Number One’ kukutana na Peter, ni yeye (Peter) ndiye aliyeanza kwa kumtambua Chibu na kuanza kuzungumza mawili matatu. Peter anadaiwa kumweleza staa huyo kuwa anamkubali na kama vipi wanaweza kupiga ngoma moja pamoja.

10852802_1435525646737573_2047207065_n
Inabidi tufanya kazi aisee: Diamond na Peter wakibadilisha contacts

Baada ya kukutana na pacha mwingine wa kundi hilo, Paul kwenye hoteli waliyofikia, Paul anadaiwa kumwambia Diamond kuwa anazipenda ngoma zake ‘Ntampata Wapi’ na ‘Mdogo Mdogo’.

Kuna video pia iliyowekwa Instagram inayomuonesha Peter akipiga gitaa na Diamond akiimba freestyle.

10903542_758690200875678_2113189746_n

10919365_752872104798136_324780829_n
Diamond na Fally Ipupa

Chanzo: MillardAyo.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents