Burudani

P-Funk kuirejesha label ya Bongo Records kwa kusaini wasanii wapya

Studio ya Bongo Records iliyo chini ya producer mkongwe P-Funk Majani inatafuta wasanii wapya.

10514111_1426513977637040_277138636_n

Majani anataka wasanii wenye vipaji wamtumie kazi zao na wale wenye bahati watakuwa chini ya usimamizi wa Bongo Records. “Bongo Records is looking for new Talent. Plz send ur demo’s to [email protected] ( Plz include a photo of ur self,” ameandika Majani.

Majani amezungumza na Bongo5 kufafanua zaidi:

“Natafuta wasanii kama watano hivi, wakufoka, wakuimba, producers, sio wa kiume tu hata wa kike pia so kama kuna mwimbaji wa kike wa kiume wote nawahitaji nataka kuchanganya changanya nitengeneze kundi fulani hivi,” amesema.

“Hao wote ni label ya Bongo RecordS ambayo ilikuwa zamani, ilikuwa label na inasifa kubwa Bongo recordS kujenga wasanii, imejenga malejendari wote ambao wanafanya vizuri kwenye muziki wa Tanzania huu. Unajua mfumo wa biashara ulikuwa umepotea, zamani kilichokuwa tunafanya ni kuuza makanda, sasa ilikuja ikapotea ikabaki wasanii wanajipatia maslahi kwa show. Unajua unapofanya kazi biashara yoyote unaweka jasho lako unategemea urudishe, inaonekana na mfumo wa sasa hivi kuna opportunity nyingi sana za kuendesha label na nimegundua kwamba bila label hatuwezi kuendesha vitu vikubwa. Zamani nakumbuka tulikuwa na matamasha tunafanya vitu vikubwa, sasa hivi kama watu wamesambaratika, tukifanya ngoma moja moja itatupotezea sio kwa mabaya kwa manufaa ya muziki. Hakuna mtu ambaye alikuja kuiga mfumo wangu baada ya mimi. MJ amefanyafanya lakini sio kama ile label. Zamani ukiambiwa bongo record ilikuwa mshtuko kwa watu. Kwahiyo wasanii watume demo za nyimbo zao, pamoja na picha, muonekano ni kitu cha umuhimu. Pia nahitaji producers na wao watume beatz zao.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents