Habari

P-Funk awakusanya maprodusa wote wakali Tanzania kuiandaa No Name 12/12/12

Producer mkongwe nchini na God father wa Bongo Flava kama anavyojulikana kwa sasa, P-Funk Majani yuko busy kuliko kawaida akiandaa kile anachokiita No Name 12/12/12. Japo bado hajaweka wazi No Name 12/12/12 ni kitu gani hasa lakini inavyoonekana ni compilation albam ya Bongo Records ambayo huenda ikatoka December 12 mwaka huu.

Katika kuikamilisha, Majani amekusanya maproducer kibao ambao wamechangia beat zao huku Master pekee ndiye aliyebakia.

“Brah! Everybody has made a beat 4 No Name except u!! Dully,Dunga,ludigo,Akil the Brain,lamar,John Mahundi,Majani,Ema wa THT,” ametweet Majani.

Naye Master J amejibu, “ Im on it bra, call u in a few days, cheers,” na mwisho Majani kumalizia kwa kutweet,“thats wat the No Name team wants to hear from the legend. Cheers Brah!

Huenda hivi karibuni Majani ataitangaza pia orodha ya wasanii watakaosikika kwenye No Name 12/12/12!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents