Michezo

Oscar Pistorius na Reeva Steenkamp hawakuwahi kufanya mapenzi – asema Mama Reeva

Oscar Pistorius na aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp hawakuwahi kufanya mapenzi, mama yake, June Steenkamp ameandika kwenye kitabu chake.

Oscar na Reeva
Oscar na Reeva

Kwenye kitabu hicho, “Reeva: a Mother’s Story”, June Steenkamp aliandika kuwa binti yake alimueleza kuwa pamoja na kwamba walilala pamoja, hawakuwahi kufanya mapenzi sababu Reeva hakutaka kuupeleka uhusiano wao katika kiwango hicho.

Pistorius alihukumiwa miaka mitano jela kwa kumuua Steenkamp bila kukusudia. Alidai alimpiga risasi kupitia mlango wa choo nyumbani kwake Pretoria, February 14, 2013, akidhania ni jambazi.

Gazeti la Sunday Times limeandika kuwa June Steenkamp ameandika kwenye kitabu chake kuwa haamini story hiyo Pistorius. “Alisema kuvuta trigger ilikuwa ajali, Nini? Mara nne ni ajali? Alisema Reeva hakupiga kelele, lakini nina uhakika alipiga kelele. Namjua binti yangu kwakuwa alikuwa na sauti sana,” ameandika kwenye kitabu hicho.

“Hakuna shaka kwenye fikira zetu kuwa kitu kibaya kilitokea, kitu kilichomuudhi Reeva kiasi cha kujificha nyuma ya mlango uliofungwa na simu mbili za mkononi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents