Michezo

Oscar Pistorius apatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake bila kukusudia

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp bila kukusudia.

Oscar-Pistorius-main

Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa katika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake.

Alisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp na hakutekeleza mauaji hayo kwa makusudi.

Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani jijini Johannesburg.
Kwa uamuzi huo wa jaji, Oscar atahukumiwa miaka michache zaidi ya jela tofauti na kama angepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.

Hukumu ya kuua bila kukusudia nchini Afrika Kusini ni hadi miaka 15 jela. Jaji Masipa aliamua kuwa waendesha mashtaka wa serikali walishindwa kutoa ushahidi wa kutosha kuwa alimuua mpenzi wake kwa kukusudia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents