Habari

Orodha ya Mahakimu na Majaji waliovuruga kesi za wauza unga kutua kwa Jaji Mkuu

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya sasa imeshika kasi, ambapo kila mtu ameelekeza masikio yake kutaka kujua nini kinajiri kila kukicha. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Dkt. Rogers William Sianga ametangaza kuanza na majaji na mahakimu waliovuruga kesi zinazohusu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Tamko hilo limetolewa alipokabidhiwa majina 97 ya wafanyabiashara wa kubwa wanaojihusisha na madawa ya kulevya kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Kamishna Sianga amesema kuna mahakimu na majaji ambao wamekuwa wakivuruga kesi za watuhumiwa wa dawa za kulevya ambapo pia amesema watapitia kesi zote za madawa ya kulevya ili kuwabaini na kisha watapeleka orodha kamili katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.

Alitolea mfano wa kesi ambazo amedai zilivurugwa na mahakimu na kuitaja moja ambapo ushahidi ulikuwa wazi kuwa mtuhumiwa amemeza dawa za kulevya, lakini hakimu akasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na matatizo ya vidonda vya tumbo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kuendelea na mapambano juu ya watumiaji wa dawa hizo, sambamba na kuwapatia matibabu ili kuokoa taifa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents