Burudani

Ommy Dimpoz kuwalipa deni mashabiki kwa kufanya video ya ‘Tupogo Remix’

Ommy Dimpoz ameamua kufanya remix ya hit song yake ‘Tupogo’ambayo alimshirikisha staa wa Nigeria J. Martins, wimbo ambao licha ya kufanya vizuri lakini uliacha deni la video ambayo ilishindikana kufanyika.

ommy

Meneja wa Dimpoz ajulikanaye kama Mubenga amezitaja sababu za kuamua kufanya remix ya wimbo huo, pamoja na mipango ya kuifanyia video.

“Sababu kubwa kwanza ya kufanya remix ya huu wimbo (Tupogo), ni wimbo ambao ulikuwa umependwa sana katika nyimbo zetu,”
Mubenga aliiambia E-News ya EATV. “na katika nyimbo ambazo zimehit haraka basi Tupogo imehit haraka sana. Kwahiyo ni wimbo mkubwa ambao nafikiri ulipendwa kwa haraka, na kwa kuwa kila sehemu ambayo tulikua tukienda tulikua tukiulizwa video video video unajua ilikua inatuumiza sana, na mimi katika usimamizi wangu waga ndio napenda kukosolewa…kwasababu huwezi kujua kila kitu, lakini moja ya vitu vilivyokuwa vinaumiza nilivyokuwa naulizwa video ya Tupogo vipi. Kwahiyo this time around tumeamua kufanya remix kwaajili ya kuifanyia video moja kwa moja”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents