Burudani

Ommy Dimpoz kumtambulisha ‘Nedy Music’ akiwa na video aliyoshoot Justin Campos

Staa wa muziki Ommy Dimpoz kupitia lebo yake ya ‘Poz Kwa Poz Entertainment (PKP)’ Mei 5 atamtambulisha ramsi msanii mpya ‘Nedy Music’ ambaye tayari ameshashoot video mpya ya wimbo ‘Usiende Mbali’ na Justin Campos wa Afrika Kusini.
ommy.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, Meneja wa PKP, Mubenga anasema kupitia bosi wa lebo hiyo, Ommy Dimpoz amemsainisha msanii huyo na Mei 5, mwaka huu, ataibuliwa.

“Tunatarajia kuachia video mpya ambayo kwa mara ya kwanza tangu tumemchukua tunatoa kazi yake, wimbo unaitwa ‘Usiende Mbali’ na audio tumefanyia pale kwa Nahreel Industry na video tumefanyia Afrika Kusini kwa Director Justin Campos,” anasema Mubenga

Ommy Dimpoz kwa sasa anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Achia Body’ ambao umepata nafasi ya kuingia kwenye chart mbalimbali za muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents