Habari

Ommy Dimpoz kuanza kusimamia wasanii chipukizi kupitia kampuni yake ya PKP

Pamoja na mafanikio anayoendelea kuyapata msanii Faraji Nyembo aka Ommy Dimpoz kupitia muziki, lakini hajasahau kule alikotokea na ndio sababu na yeye kupata wazo la kuanza kuwasaidia wasanii w
achanga.

ommy

Ommy ambaye weekend iliyopita alikata kiu ya mashabiki wa jiji la London, Uingereza katika show iliyofanyika siku ya Valentine, amesema ana mpango wa kuanza kusimamia wasanii chipukizi kupitia kampuni yake ya PKP.

“PKP ni Poz kwa Poz ambayo ina vitu vingi ambavyo vya mavazi lakini pia baadaye itakuwa inasimamia wasanii,” Ommy Dimpoz aliiambia E-News ya EATV. “Lakini kutakuwa na official launch ambayo itakuwa na mambo mengi kwahiyo si vizuri kuviongelea vitu ambavyo tayari viko kwenye mipango kama hivi unaweza ukatolewa nje ya mpango. Kwahiyo najadiliana na management yangu nione tutafanya kitu gani.”

Kabla ya kuwa msanii anayejitegemea, Ommy alikuwa akiimba na bendi ya TID, Top Band.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents