Burudani

Ommy Dimpoz kuachia album pamoja na bidhaa za PKP katika msimu wa Valentine 2014

Hitmaker wa Tupogo, Ommy Dimpoz amesema anatarajia kutoa album na bidhaa za zake PKP katika msimu wa Valentine Day mwakani (2014) ingawa hakuna soko la album.

Ommy Dimpoz akicheza Tupogo

Akizungumza na Clouds FM leo, Ommy amesema katika harakati zake za muziki sehemu mbalimbali amekuwa akiombwa na kuulizwa kuhusu suala la album pamoja na product za PKP.

“Product za PKP zipo kiwandani zinafyatuliwa,kwahiyo itakavyokuwa tayari nitawaambia, kwasababu mwakani target zaidi ni msimu wa Valentine tutalaunch vitu vingi nini na nini kazi mpya kuna vitu vingi vinakuja. Pia natarajia kuachia album kwasababu watu wanasema soko halikidhi kutoa album lakini inabidi utoe kwasababu ya fans. Kwasababu kila ninaposafiri watu wanaulizia album na nini. Kwahiyo naona sasa hivi nitoe album kwaajili ya PKP fans.Sio chini ya nyimbo 10 na za zote zilizotangulia zitapatikana na zingine mpya ambazo sijatoa,” alisema Dimpoz.

“Nitatoa bila kujali hasara niuze nisiuze poa,kwasababu soko sasa hivi album haziuziki na lazima msanii katika profile uwe na album. Kwahiyo natoa kwasababu watu wanahitaji album. Kuna watu wana nia ya kuwa na kazi yako sasa ukianza kusema ‘ohh sasa album hazilipi’ unaanza kuwaangusha mashabiki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents