Burudani

Ommy Dimpoz atoa sababu za kwanini hajawahi kumtambulisha hadharani mpenzi wake

Wapo baadhi ya wasanii wa Tanzania ambao wameamua kuweka wazi mahusiano yao kwa kuwatambulisha wapenzi wao kwa mashabiki kwa kupost picha zao, au hata kuwataja kwenye Interviews pale wanapoulizwa kuhusu mahusiano, na kuna wengine ambao wameamua kuweka private mahusiano yao.

Ommyz

Muimbaji wa ‘Wanjera’ Ommy Dimpoz yuko kwenye orodha ya wasanii ambao hawajawahi kuyaweka wazi mahusiano yao.

Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5 sababu za kwanini hajawahi kumtambulisha hadharani mpenzi wake.

“Sijapenda kuweka wazi sana swala la mahusiano kwasababu inatakiwa mimi niweze kuwa na uhakika kwamba huyu ambaye namtambulisha kwa wananchi ni kweli wakati umefika, kwasababu leo unaweza ukawatambulisha huyu baada ya siku tatu mambo hayaeleweki ukatambulisha mwingine, kwahiyo mwisho wa siku utaonekana kijana unatumia nafasi yako kuweza kuchezea watoto wa kike, kwahiyo najaribu kuwa makini kwa hilo lakini kipindi kitakapofika watu wataweza kufahamu kama Ommy ‘bae’ wake ni yupi” alimaliza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents