Burudani

Ommy Dimpoz atemana na meneja wake Mubenga

Aliyekuwa meneja wa PKP ya Ommy Dimpoz, Mubenga, amesema hafanyi tena kazi na muimbaji huyo wa wimbo ‘Achia Boby’ huku akiweka wazi mpango wa kuanzisha label yake mpya.
ommy-dimpoz-na-Meneja-wake-Mubengamuba
Mubenga na Ommy Dimpoz

Mubenga ambaye alifanya kazi kwa muda mrefu na Ommy Dimpoz amekiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa ameakua kuachana na PKP ili afanye mambo yake mengine.

“Kwa sasa najipanga ili kuja na kampuni yangu ambayo itaitwa Bengaz Entertainment ambayo itakuwa inahusika na maswala yote ya burudani, hivyo wadau wangu waelewe kwamba kwa sasa sifanyi kazi tena na pozi kwa pozi”.

Hata hivyo Mubenga hakuweka wazi sababu iliyopelekea yeye kuachana na PKP huku akisisitiza kuwa anarudi katika kazi zake alizokuwa akizifanya kabla ya kuungana na pozi kwa pozi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents