Burudani

Ommy Dimpoz ashauri watu kuwekeza kwenye vifaa vya kufanyia video TZ ili wasanii wasiende kushoot video zao nje

Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz ametoa majibu ya maswali ya wengi ambao huwa wanajiuliza sababu zinazowafanya baadhi ya wasanii wa Tanzania kutumia pesa nyingi kwenda kushoot video zao nje ya nchi, huku Tanzania ikiwa na maeneo mengi na mazuri ambayo bado hayajatumika.

ommy

“Biashara ya video ishaingia ushindani, kwahiyo kuna haja ya kuwekeza kwenye vifaa,” Ommy Dimpoz amefunguka kupitia 255 ya XXL.

“Mi nauhakika hapa mtu ana mavifaa kibao unaenda kushoot Lushoto huko noma, wazungu wenyewe watauliza umeshoot wapi. Tuna maeneo kibao Zanzibar wapi wapi wapi ya kushutia, sio kwamba hatuna maeneo, maeneo tunayo lakini hatujawa na vile vitu. Kwahiyo ndo maana hata mtu pia unafikiria ah sijui nishoot Zanzibar, lakini unawaza kumchukua labda GodFather au nani kumleta huku Tanzania ndio mziki.” Amesema.

Ommy Dimpoz
Ommy ameongeza kuwa zipo faida nyingi ambazo mtu atakayeamua kuwekeza kwa kuleta vifaa atazipata mbali na video, ikiwa ni pamoja na kufanya matangazo, na kukodisha vifaa hivyo ni biashara nzuri inayohitaji uwekezaji.

“Halafu mtu utakapoleta vifaa hivyo nauhakika hautaishia kwenye video tu, kuna matangazo, utakodi utafanyaje…Watu lazima waelewe kitu kimoja kwamba hakuna mtu anaependa kujitia gharama kama kuna uwezo wa kuepuka gharama, sio ufahari mi nina vitu vingi vya kufanya sio kwamba nataka tu nikalipe dola elfu 30 kushoot video wakati nina uwezo wa kuokoa hiyo hela labda kulipa dola elfu 15 au elfu 10”.

Ommy ambae video yake mpya amefanyia nchini Uingereza na mwongozaji wa Nigeria aitwaye Mr. Moe Musa, alimaliza kwa kuwashauri tena wadau wanaoweza kuwekeza:

“Wadau wanatusikia sie ndio wasanii wenyewe tunasema kwamba muziki unalipa mnaona sasa hivi vijana wenu wanapata shilingi mbili tatu, hizo shilingi mbili tatu mtagawana nao vipi kuliko kwenda kuwapa watu wengine huko nje ya nchi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents