Burudani

Ommy Dimpoz akanusha kupangiwa nyumba, aweka wazi ujenzi wa nyumba zake mbili Dar

Msanii wa muziki Ommy Dimpoz amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amepangiwa nyumba.

Aidha amedai kwa sasa anaendelea na ujenzi ya nyumba zake mbili, moja ipo Kigambani na nyingine Mbezi.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kajiandae’ amedai kwa sasa amekodi Apartment Mikocheni.

“Unajua binadamu wanaweza kuongea hiki na hiki lakini ukweli ni kwamba mimi naishi Mikocheni kwenye apartment hivyo siishi Mbezi,” Ommy alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Ila Mbezi kuna sehemu nina site yangu ambayo najenga na site nyingine ipo Kigamboni. Kwa hiyo sina nyumba ambayo nimepangisha au nimepangishiwa kwa hiyo hizo stori sijui bimkubwa sijui nini siyo kweli,”

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai muda haujafika wa kumwonyesha mpenzi wake. 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents