Michezo

Okocha ammwagia sifa Victor Wanyama

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Nigeria Jay Jay Okocha ambaye alisha wahi kuichezea klabu ya Bolton Wanderers ya Uingereza, amesema kuwa idadi ya juu ya wachezaji wa Kenya barani Ulaya itaipiga jeki timu ya taifa ya harambee stars na kuwa na mchezo mzuri.

Okocha alisema hayo wakati akiongea na runinga ya NTV nchini Kenya amesema kuwa mchezaji wa Kenya Victor Wanyama anayechezea soka yake ya kulipwa katika klabu ya Tottenham nchini Uingereza anaifanyia kazi nzuri Kenya na bara la Afrika.

”wakati wachezaji wetu wanapofanya vizuri kule Ulaya hawasemi kwamba ni mchezaji wa Kenya,wao husema mtazameni yule mchezaji kutoka Afrika, lakini twashukuru kwamba wanyama anafanya kazi nzuru sana”

Okocha amesema kuwa ni vyema kwamba mchezaji huyo anaipeperusha bendera ya Kenya juu na kwamba hatua hiyo inafaa kuwafungulia milango wachezaji zaidi wa Kenya kwenda Ulaya.

Amesema kuwa shirikisho la soka la Kenya linafaa kuchukua hatua mwafaka kwa lengo la kutumia fursa hiyo ili kuwasaidia vijana zaida kujiunga na klabu za Ulaya.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents