Habari

Ofisi ya CUF Zanzibar yavamiwa

Watu wasiojulikana maarufu kama (mazombi) wameivamia ofisi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Jimbo la Dimani wilaya ya Magharibi B.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku CUF wakitaka uchunguzi uanze mara moja kuwabaini wahalifu.

“Ni kweli taarifa tunazo za watu kuvamia ofisi hiyo ya CUF na kuwapiga pamoja na kuwahujumu watu na huo ni uharamia unaoripotiwa mara kwa mara,” alisema Kamanda Ali. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Salim Abdallah Bimani alisema, “Huu ni uvunjifu wa amani na tunataka Rais John Magufuli iwapo anayo nia ya dhati afuatilie hujuma hiyo ambayo watekelezaji wake wanajulikana lakini hawakamatwi”.

Aliendelea kuzungumza “Mazombi wameshawapiga sana wananchi hasa wafuasi wa CUF ambao hawana hatia, wengine mpaka walipoteza maisha, wameshawapiga watu na kuwajeruhi vibaya na pia kuwaibia watu mali zao na hatuoni hatua yoyote ikichukuliwa”.

Aliongeza “Tunamwambia Rais Magufuli kwa mujibu wa Katiba yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwalinda raia wote wa nchi hii, achukue hatua.” Tukio hilo lililotokea saa 6.30 usiku wa kuamkia jana.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents