Habari

Nywele za aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln zauzwa dola 25,000

Vitu vya kumbukumbu vya aliyekuwa rais wa 16 wa Marekani Abraham Lincoln vimeuzwa katika mnada mjini Dallas nchini Marekani na kupata dola 800,000.

Lincoln
Abraham Lincoln

Msokoto mmoja wa nywele za rais huyo aliyeuawa umeuzwa kwa dola 25,000 lakini barua iliyokiri kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe havikuwa vizuri haikuuzwa.

barua

Barua iliyotiwa sahihi na naibu wake John Wlkes Booth iliuzwa kwa dola 30,000 huku agizo lake la kijeshi likitia kibindoni dola 21,250.

Ukusanyaji wa vitu hivyo 300 ulianzishwa mwaka 1963 na mmiliki wa jumba la sanaa Donald Dow aliyefariki miaka mitano iliopita.
Mwanae Greg amesema kuwa ni wakati wakusanyaji wengine wapate fursa ya kuifurahia.

Amesema kuwa baba yake alikuwa ameanza ukusanyaji huo kutokana na maslahi yake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na historia ya kijeshi,lakini baadaye alikuwa na hamu na Lincoln na mauaji yake.

Chanzo: BBC

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents