Burudani

Nyimbo 5 za Chidi Benz ambazo hatutozisahau daima

Kwenye maisha ya muziki yaliyofunikwa na umaarufu kuna mambo mengi ndani yake. Vishawishi na marafiki wapya mara nyingi huwabadilisha tabia zao za halisi na kuwafanya kuwa watu wapya kwenye jamii.

Hakuna mtu yeyote kutoka mitaa ya IlaLa aliyedhani kuwa Rashidi Makwiro angefikia kwenye hali ambayo anayo leo hii ila yote ni matokeo ya maisha ya umaarufu kwa vijana wengi. Watu wengi walishtuka baada ya kumuona kwenye jukwaa la Fiesta hali yake kimwili haikuwa nzuri kama wakati ule alivyotoka sober house Bagamoyo.

Wakati ule alionekana afadhali alikuwa na muonekano mzuri na pengine angeongeza bidii kidogo angeweza kuurudisha ule mwili wake wa zamani Chidi Benz aka Chuma. Chidi Benz hayupo kwenye ubora wake kimuziki ila hiyo bado haijafanya watu wazisahau hit zake kali alizowahi kufanya kwenye Bongo Flava na mambo mengi mema aliyoufanyia muziki huu.

Akiwa na tuzo zaidi ya 5 za msanii bora wa hip hop na wimbo bora wa hip hop haikuwahi kuwa kitu rahisi kwa wakati ule kwenye game ambayo ilikuwa imetawaliwa na wakali wengi kwenye Hip hop ila haikuwa jambo gumu kwa mchizi huyu wa IlaLa Maghorofani wenyewe wanapaita La Familia kutusua na kuzibeba zile awards kama hana akili nzuri.

Makala hii inakuletea ngoma 5 kali za muda wote ambazo zimewahi kufanywa na Chidi Benz wa Ilala.

Ngoma Itambae (Dar es Salaam Stand Up)

Wimbo bora wa Rap kwenye Kilimanjaro Music Awarda 2009. Beat nzuri kutoka kwa Pancho Latino pale Dhahabu Records kwa Dully ilitendewa haki vya kutosha na sauti nzito yenye mamlaka kutoka kwa Chidi Benz. Ni wimbo uliofungua mambo mengi kwa Pancho Latino na mpaka leo bado umebaki kuwa wimbo mkubwa zaidi kuwahi kutengeneza huku ukibaki wimbo bora zaidi kutoka kwa Chidi Benz. Sauti ya Lameck Ditto ilisikia pia kwenye wimbo huu.

Mmenisoma

https://www.youtube.com/watch?v=mOEeOonzTbQ

Hivi unajua kuwa wimbo ule ulikuwa unazungumzia janga la ukimwi?! Sio rahisi kujua kutoka kwenye jina la wimbo, beat nzuri ya kuchezeka kutoka kwa P.Funk Majani wa Bongo Records ingekufanya kudhani ni wimbo fulani hivi wa kuruka ukiwa club.

Verse ya kwanza ya ule wimbo Chidi Benz anazungumzia mambo ya starehe huku verse ya pili na ya tatu akiwaasa vijana wenzie umuhimu wa kuwa waaminifu na kutumia kinga. Ni wimbo uliomfanya Chidi Benz achukue tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop mwaka 2010. Sauti ya Maunda Zorro inasikika pia kwenye wimbo huu.

Naitwa Nani

Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lyinn alikuwepo kwenye kiitikio cha wimbo huu. Dunga kwenye beat kutoka pale 41 Records/Mandugu Digital ilipelekea wimbo huu kumfanya Chidi Benz aondoke na tuzo ya msanii bora wa hip hop kwenye Kilimanjaro Music Award smwaka 2006.
Ilikuwa ni tuzo ya kwanza kwa Chidi Benz na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuchaguliwa kwenye tuzo zile ila alifanya maajabu na toka pale alifungua njia yake na kwenda kumfanya awe mmoja kati ya wasanii bora wa hip hop wa muda wote.

Hasira za nini

Alikiba wakati huo kabla hajawa King Kiba alikuwepo kwenye ngoma hii. Kutoka pale G.Records kwa KGT wimbo huu ulikwenda kuwa wimbo mkubwa kwenye maisha ya Chidi Benz. Sauti tamu ya Alikiba kwenye chorus na back vocals, ulimfanya Chidi Benz awe kipenzi cha wasichana wengi na kumfanya awe ni rapper anaeweza kubadilika apendavyo. Ilikuwa mwaka 2007 ila mpaka kesho usikiliza wimbo huu bado unakupa hisia zile zile.

Mashallah

https://www.youtube.com/watch?v=ui3nWUlTHY8

Hapa nilipata kigugumizi kikubwa mno.Wimbo gani ulistahili kufunga list hii ya mkongwe Chidi Benz?! Kumchukua Mfalme wa Taarabu Alhadji Mzee Yusuph alikuwa jambo rahisi kwa wakati ule japo yeye hakuwa wa kwanza kufanya hivi ila ilileta kitu kikubwa mno kwenye maisha ya Chidi Benz ila mwisho wa siku ulikwenda kuwa wimbo mkubwa na kila mtu alifurahiswa nao.

Miika Mwamba alitengeneza beat fulani ya taratibu.Bila shaka huu ulikuwa ni wimbo wa mwisho mkali zaidi Kutoka kwa Chidi Benz inshallah Mungu amtilie wepesi arudi kwenye uzima wake wa afya na akili arudishe makali yake na arudi kwenye siku zake za ubora.

By Heri Lukaku Chelsea (Facebook)
Instagram:Heri_Lukaku_Chelsea

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents