Habari
Nyerere day
Leo tunatimiza miaka 11 tangu baba wa Taifa hili Mwl J.K.Nyerere ambaye alitutoka mwaka Octoba 14, 1999 na leo tunaikumbuka tena siku hiyo kama Nyerere Day.
Hii ni changamoto kwa Watanzania ambao tunatimiza miaka 50 ya uhuru, pia tunapaswa tujiulize tumeendeleza kipi, kati ya vile alivyotuachia mwalimu. Pia huu ni muda wa kujiuliza je? tunamuenzi mwalimu kwa lipi, hasa katika ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuuenzi muungano wetu. Mwalimu Nyerere anaheshimiwa na watanzania hadi na maitaifa ya nje kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko kutumikiwa, je Viongozi wa sasa wapo hivyo?
Mwl akitangaza uhuru kamili….. kwa Tanganyika
Mwl akiwa na viongozi wa dini………….
Msafara tayari kwaajili ya kufanikisha safari ya mwisho ya baba wa Taifa…
Mwl akisaliwa kwenye kanisa la St Joseph Poster ya zamani…………
Na haya ndiyo makazi ya kudumu kwa mwalimu…….