Burudani

Nora: Wema, Lulu, Wolper wanaweza, Batulli, Aunt Ezekiel, Chuchu Hans hamna kitu!

Muigizaji wa filamu nchini, Nuru Nassoro maarufu kama Nora anaweza akawa ameshaongeza matatizo mengi kuyazidi 99 ya Jay Z.

Kwenye kipindi cha hivi karibuni cha Mkasi, Salama Jabir alimuuliza swali gumu kwake la kuwataja wasanii wa filamu wanaofaa na wasiofaa. Nora alikataa kutaja akijitetea kuwa hataki beef na mtu lakini watangazaji wa show hiyo walimrahisishia kazi na kuanza kuwataja ‘randomly’ waigizaji mbalimbali na kumtaka aseme tu kama wanafaa ama hawafai.

Hivyo ndivyo alivyojibu na kuwapa makavu live anaohisi wanafaa kurudi ‘kuflip burger’ na kuacha kuigiza.

Kajala – Hapana
Batulli – Hamna kitu
Steve Nyerere – Hapana
Wema Sepetu – Yeah anafaa
Rose Ndauka – Anafaa vibaya mno
Wolper – anajaribu… anafaa
Aunt Ezekiel – Hamna Kitu
JB – Anaweza
Hemed – Anaweza
Mlela – Hapana
Lulu – Ndiyo
Irene Paul – Anaweza
Chuchu Hans – Hamna Kitu

Unakubaliana na Nora?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents