Promotion

NMB yawezesha mkutano wa wasambazaji mafuta na gesi nchini Tanzania

Mwishoni mwa wiki NMB ilifadhili mkutano wa makampuni na taasisi ambazo wamepewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na gesi nchini. Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam kwa siku mbili ukiambatana na maonyesho ya biashara kutoka makampuni tofauti nchini Tanzania.

1 (2)
Mkuu wa kitengo cha huduma za miamala kwa taasisi NMB, Gerald Kamugisha akielezea jinsi NMB inavyoweza kusaidia makampuni na taasisi mbali mbali zinazosambaza mafuta na gesi nchini Tanzania

2 (2)
Kamishina wa Nishati na masuala ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise, akimkabidhi cheti Mkuu wa kitengo cha huduma za miamala kwa taasisi NMB, Gerald kamugisha kwa udhamini ambao NMB umetoa ili kufanikisha mkutano huo.

Dhumuni kubwa la mkutano huu lilikuwa ni kutengeneza mahusiano baina ya wafanya biashara na kujadili jinsi ambavyo huduma zitolewazo na makampuni na taasisi zilizopewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na gesi nchini zinavyoweza kuisaidia jamii husika.

3 (2)
Meneja ukuzaji wa biashara NMB, Masato Wasira akiwaelezea baadhi ya washiriki wa
mkutano huo juu ya huduma zitolewazo na benki ya NMB

4 (2)
Sehemu ya washiriki wa mkutano wakisikiliza kwa makini

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents