Promotion

NMB yashirikiana na Tigo Pesa kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake

Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi Tigo wamezindua huduma ya kuweka na kutuma pesa kupitia simu za mkononi. Lengo kubwa la huduma hii ni kuwezesha huduma za kibenki kuwafikia wateja kwa ukaribu na urahisi zaidi.

1
Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa kitengo cha Athari wa NMB, Tom Borghols (kati) na Mkuu wa kitengo cha huduma ya Tigo Pesa, Ruan Swanepoel wa kwanza (kulia) wakiweka sahihi mkataba wa kutoa huduma za NMB kwa kupitia Tigo Pesa . Huduma ambayo inamwezesha mteja wa NMB mobile kutuma fedha kwenda Tigo Pesa na mteja wa Tigo Pesa kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB. Kushoto akishuhudia ni Mkuu wa kitengo cha Huduma Binafsi wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela

Huduma hii mpya inawawezesha wateja wote wa NMB na Tigo kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Tigo Pesa kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Vilevile, mteja anaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Tigo Pesa. Huduma hii inafanyika kwenye simu za mkononi na utoaji wa fedha unafanyika kwa Wakala yeyote wa Tigo Pesa.

DSC_3690
Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa kitengo cha Athari wa NMB, Tom Borghols (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha huduma ya Tigo pesa, Ruan Swanepoel wakibadilishana mkataba wa ushirikiano utakao muwezesha mteja wa NMB mobile kuweka na kuchukua pesa zake mahali popote kupitia mawakala wa Tigo Pesa nchini na mteja wa Tigo Pesa kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents