Burudani

Nitamwanika mume wangu lakini sio mpenzi wangu – Dayna Nyange

Dayna Nyange amefunguka sababu ya kuyaweka siri maisha yake ya mahusiano.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu zake binafsi na hata yeye hapendi mpenzi wake amuweke wazi mitandaoni ila atakuja kufanya hivyo kwa mume wake na sio kwa mpenzi.

“Nimekuwa msiri kwenye mahusiano kwa sababu kadhaa. Nilishasema nitampost mume wangu, kumpost mpenzi wangu au mtu wangu ambaye nipo naye sio kama ndio ishara kuwa nampenda au ananipenda sana na hata yeye sijawahi kumwambia anipost wala sitamani hilo,” amesema Dayna.

Hitmaker huyo wa Komela ameongeza kuwa haitarudia tena yeye kuwa na mahusiano na msanii mwenzake au mtu yoyote maarufu japo ilishawahi kutokea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents