Diamond Platnumz

‘Nitafute ukipata nafasi’ meneja wa Trey Songz na Mariah Carey amwambia Diamond

Sio rahisi kuambiwa na meneja wa Trey Songz, Mariah Carey na Big Sean ‘nitafute ukipata nafasi’, kama hauna kitu cha maana unachoweza kufanya.

Kevin na Diamond

Lakini kwa Diamond hilo linawezekana. Muimbaji huyo wa ‘Mdogo Mdogo’ jana alifanikiwa kupata comment muhimu zaidi kwenye Instagram tangu ajiunge na mtandao huo baada ya aliyewahi kuwa makamu wa rais wa Def Jam Recordings, Kevin Liles na ambaye hivi karibuni alichukua nafasi ya Jermaine Dupri kama meneja wa Mariah Carey, kucomment kwenye picha ya Diamond.

Screenshot_2014-08-18-12-39-11

“Great shot. Hit me when you get a chance,” aliandika Kevin kwenye picha ya Diamond (hiyo chini aliyoweka Instagram).

10575981_1468191006764794_277656629_n

“l am grateful, lemmie do it ryt now boss,” alijibu Diamond.

DIAMOND na Kevin
Diamond Platnumz na Kevin Liles walikutanishwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi June nchini Marekani

“Ilikuwa ni namna ya kuangalia nafanya vipi katika soko la Amerika na dunia nzima” Diamond aliimbia Bongo5 kuhusiana na kukutana na Kevin.

“So nilipokutana na mheshimiwa Rais akaniambia kitu gani unahitaji nikusaidie, nikamwambia connection, kila kitu ni connection njia ya kuweza kuingia katika soko la Amerika na dunia nzima, so akasema basi nitakukutanisha na mtu fulani ambaye naamini anaweza akakusaidia, so akamtafuta akampigia simu nikaonana naye(Kevin Liles)”.

Katika hatua nyingine mshindi huyo wa tuzo 7 za KTMA 2014, aliiambia Choice FM mwanzoni mwa mwezi huu kuwa mashabiki wake wategemee kupata zawadi ya wimbo aliomshirikisha msanii mkubwa wa Marekani. “Wategemee pia collabo nyingi sio kutoka Afrika, kutoka nje ya Afrika kabla ya mwaka haujaisha,” alisema Diamond japo alikataa kusema ni msanii gani.

Hivyo mawasiliano na Kevin Liles yanatoa dalili kuwa collabo hiyo inaweza kuwa kati yake na Trey Songz ama msanii mwingine anayesimamiwa na nguli huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents